Featured Post

fahamu kitu kuhusu mwalimu nyerere baba wa taifa la tanzania

                                                          Tokeo la picha la nyerere photo                                                                                 Jump to navigationJump to search Mwalimu Julius Nyerere Rais wa Tanzania Muda wa Utawala 26 Aprili 1964 – 5 Novemba 1985 Waziri Mkuu Rashidi Kawawa (1972–77) Edward Sokoine (1977–80) Cleopa Msuya (1980–83) Edward Sokoine (1983–84) Salim A. Salim (1984–85) Makamu wa Rais Abeid Karume (1964–72) Aboud Jumbe (1972–84) Ali Hassan Mwinyi (1984–85) aliyemfuata Ali Hassan Mwinyi Rais wa Tanganyika Muda wa Utawala 9 Desemba 1962 – 25 Aprili 1964 Waziri Mkuu Rashidi Kawawa Waziri Mkuu wa Tanganyika Muda wa Utawala 1 Mei 1961 – 22 Januari 1962 Monarch Elizabeth II mtangulizi Ofisi iliundwa aliyemfuata Rashidi Kawawa Waziri Kiongozi wa Tanganyika Muda wa Utawala 2 Septemba 1960 – 1 Mei 1961 Monarch Elizabeth II tarehe ya kuzaliwa 13 Aprili 1922 Butiama, Tanganyika tarehe ya kufa 14 Oktoba 1999 (umri 77) London, Uingereza mahali pa kuzikiwa Butiama, Tanzania utaifa Mtanzania chama CCM ndoa Maria Nyerere watoto 7 mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere Chuo Kikuu cha Edinburgh Fani yake Mwalimu dini Ukristo (Katoliki) tovuti juliusnyerere.info Historia ya Tanzania Coat of Arms of Tanzania This article is part of a series Uendo Historia ya Zanzibar Ukoloni Mgawanyo wa Afrika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani Mkataba wa Zanzibar-Helgoland Mkwawa Vita vya Maji Maji Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki Tanganyika Uhuru Mapinduzi ya Zanzibar Julius Nyerere Ujamaa Tamko la Arusha Vita vya Kagera Ali Hassan Mwinyi Benjamin Mkapa Jakaya Kikwete {Kigezo:Data99 Tanzania Portal omh Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Butiama, mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 - London, Uingereza, 14 Oktoba 1999) alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "baba wa taifa". Kwa hakika aliiathiri kuliko yeyote yule. Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha. Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu." Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, halafu kama rais; baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais. Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi katika nchi. Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Kwa ruhusa ya makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Jimbo Katoliki la Musoma linashughulikia kesi ya kumtangaza mwenye heri na hatimaye mtakatifu. Kwa sababu hiyo anaitwa pia "mtumishi wa Mungu". Yaliyomo 1 Maisha yake 2 Mafanikio 3 Ukosoaji dhidi yake 3.1 Sifa zake 4 Heshima na Tuzo 4.1 Nishani 4.2 Tuzo 5 Machapisho ya mwl.Julius K. Nyerere 6 Marejeo 7 Viungo vya nje Maisha yake Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika). Alikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusomea shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake. Mapadri wakiona akili yake kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945. Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uskoti, Ufalme wa Muungano, akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika). Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika. Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. Alijiuzulu ualimu[1] na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah. Julius Nyerere akiwa mzee mnamo mwaka 1977. Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza. Nyerere aliendelea kuongoza taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi. Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi. Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W. Mkapa kama mgombea wa urais mwaka 1995, ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi. Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi. Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu. Mafanikio Nyerere akichanganya udongo wa Zanzibar na Tanganyika wakati wa muungano mwaka 1964. Kati ya mafanikio makubwa ya Nyerere kuna: kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo kudumisha amani ya muda mrefu tofauti na hali ya nchi jirani, iliyofanya Tanzania iitwe "kisiwa cha amani". Pia kustawisha utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda. Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile: Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo). Ukosoaji dhidi yake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Nyerere analaumiwa kwa siasa yake ya kiujamaa kuwa ilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania. Siasa yake ya ujamaa ilishindikana kwa kiasi kikubwa baada ya mwaka 1976 kwa sababu mbalimbali za nje na za ndani ya nchi. Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa ya kijamaa na kuwa hataweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa nyingine ambazo yeye hakuwa na imani nazo, Nyerere kwa hiari yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais kuanzia uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani Ali Hassan Mwinyi, aliyetawala kwa siasa ya uchumi wa soko huria. Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere katika tafrija ya kumwaga alitamka juu ya siasa yake upande wa uchumi: “Nimefeli. Tukubali hivyo.” Kosa lingine ambalo wengine wanaona Nyerere alilifanya ni kumhadaa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Abeid Amaan Karume kwa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kuanza kupora mamlaka ya Zanzibar kidogokidogo. Kwa hivi sasa Wanzanzibari wengi wamechoka na Muungano huo, na wanataka uhuru wa nchi yao ili wapumue. Hata upande wa bara wananchi wengi wanalalamikia kutoweka kwa Tanganyika na serikali yake. Pia kuna makundi ya Waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya dini yao na kupendelea Wakristo katika utoaji wa elimu na madaraka,japo wasomi wengi kwa kipindi cha utawala wake walikuwa Wakristo. Sifa zake Nyerere akicheza bao kwake Butiama, akitazamwa na mwandamizi wake katika urais Ali Hassan Mwini, mke wake Mama Maria, na kaka yake, chifu Burito. Pamoja na hayo, Nyerere bado anakumbukwa na Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu. Pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika barani kote hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika. Ni mmoja wa viongozi wachache waadilifu waliokwepa kujilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24. Kaburi la Nyerere kijijini Butiama. Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) akafariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba 1999. Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama. Heshima na Tuzo Nishani Nishani Nchi Mwaka Ref Ribbon jose marti.png Nishani ya José Marti Bendera ya Kuba Cuba 1975 [2] MEX Order of the Aztec Eagle 1Class BAR.png Nishani ya Tai ya Kiazteki (Ukosi) Bendera ya Mexiko Mexiko 1975 [3] Medalha Amílcar Cabral.svg Nishani ya Amílcar Cabral Bendera ya Guinea-Bisau Guinea Bissau 1976 [3] Nishani ya Eduardo Mondlane Bendera ya Msumbiji Msumbiji 1983 [3] Ordem Agostinho Neto.svg Nishani ya Agostinho Neto Bendera ya Angola Angola 1985 [3] Order of the Companions of O.R. Tambo (ribbon bar).gif Nishani ya Masahaba wa O. R. Tambo (Dhahabu) Bendera ya Afrika Kusini Afrika Kusini 2004 [4] Nishani ya Kifalme cha Munhumutapa Bendera ya Zimbabwe Zimbabwe 2005 [5][6] Order of the Pearl of Africa (Uganda) - ribbon bar.gif Nishani Ubora wa Lulu ya Afrika (Bwana tukufu) Bendera ya Uganda Uganda 2005 [7] Order of Katonga (Uganda) - ribbon bar.png Nishani ya Katonga Bendera ya Uganda Uganda 2005 [7] National Liberation Medal (Rwanda) - ribbon bar.png Medali ya Ukombozi wa Kitaifa Bendera ya Rwanda Rwanda 2009 [8] Campaign Medal Against Genocide (Rwanda) - ribbon bar.png Medali ya Kampeni Dhidi ya Mauaji ya Kimbari Bendera ya Rwanda Rwanda 2009 [8] Order of the Most Ancient Welwitschia Mirabilis (Namibia) - ribbon bar.gif Nishani ya Kikale cha Welwitschia Mirabilis Bendera ya Namibia Namibia 2010 [9] Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanzania) - ribbon bar.png Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bendera ya Tanzania Tanzania 2011 National Order of the Republic (Burundi) - ribbon bar.png Nishani ya Kitaifa cha Burundi Bendera ya Burundi Burundi 2012 [10] Order of Jamaica.gif Nishani ya Jamaika Bendera ya Jamaika Jamaika [11] Tuzo 1973: Jawaharlal Nehru Award for International Understanding[12] 1982: the Third World Prize 1983: Nansen Refugee Award 1986: Sir Seretse Khama SADC Medal 1987: Lenin Peace Prize 1988: Joliot-Curie Medal of Peace 1992: International Simón Bolívar Prize 1995: Gandhi Peace Prize Kisha kufa 2000: Statesman of the 20th century by the Chama cha Mapinduzi 2009: World Hero of Social Justice by the 63rd President of UNGA, Miguel d'Escoto Brockmann[13] 2011: Tanzania Professional Network Award[14] Machapisho ya mwl.Julius K. Nyerere Freedom and Unity (Uhuru na Umoja): Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1952–1965 (Oxford University Press, 1967) Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1965-1967 (1968) Ndamo zimo: "The Arusha Declaration"; "Education for self-reliance"; "The varied paths to socialism"; "The purpose is man"; and "Socialism and development." Freedom & Development (Uhuru na Maendeleo). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1968-73 (Oxford University Press, 1974) Ndani zimo mada za elimu kwa watu wazima; uhuru na maendeleo; kujitegemea; na miaka kumi ya uhuru. Ujamaa - Essays on Socialism' (1977) Crusade for Liberation (1979) Julius Kaisari, Tafsiri ya mchezo wa William Shakespeare unaoitwa Julius Caesar Mabepari wa Venisi, Tafsiri ya mchezo mwingine wa William Shakespeare, The Merchant of Venice Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Mathayo, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Mathayo Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Marko, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Marko Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Luka, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Luka Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Yohana, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Yohane Utenzi wa Matendo ya Mitume, Tafsiri ya kishairi ya Matendo ya Mitume Marejeo ↑ Barua ya kujiuzulu ualimu ya Julius Kambarage Nyerere ↑ Condecorado Julius K. Nyerere por el Gobierno Revolucionario con la Orden Nacional Jose Marti LANIC [LATIN AMERICAN NETWORK INFORMATION CENTER] (Granma) (Kihispania) ↑ Jump up to: 3.0 3.1 3.2 3.3 Awards / Prices Juliusnyerere.info ↑ Government Gazette (PDF) (Kiingereza accessdate=26 Septemba 2013). info.gov.za (11 June 2004). ↑ Maura Mwingira (18 April 2005). Nyerere awarded Zimbabwe’s highest medal. Kafoi.com (Daily News (Harare)). Iliwekwa mnamo 17 June 2013. ↑ The Royal Order of Munhumutapa (Kiingereza accessdate=26 Septemba 2013). SADC Today (4 October 2005). ↑ Jump up to: 7.0 7.1 "Museveni honours Nyerere", 10 July 2007. (Kiingereza accessdate=26 Septemba 2013) ↑ Jump up to: 8.0 8.1 Daniel R. Kasule. "Museveni, Zenawi, Nyerere to receive national honours", The New Times, 3 July 2009. (Kiingereza accessdate=26 Septemba 2013) ↑ Tanganyika: Africa’s mecca for liberation movements Archived from the original on 16 May 2013 ↑ Museveni gets prestigious Burundi award (Kiingereza accessdate=26 Septemba 2013). New Vision (4 July 2012). ↑ Members of the Order of Jamaica (Deceased). Government of Jamaica. Iliwekwa mnamo 26 September 2013. ↑ List of the recipients of the Jawharlal Nehru Award. Indian Council for Cultural Relations. Iliwekwa mnamo 8 February 2013. ↑ Morales Named “World Hero of Mother Earth” by UN General Assembly. Latin American Herald Tribune. Iliwekwa mnamo 8 February 2013. ↑ Kikwete urges local experts to embrace integrity. Daily News (4 December 2011). Iliwekwa mnamo 9 February 2013. Viungo vya nje Taasisi ya Mwalimu Nyerere Contemporary Africa Database - People/ Nyerere http://www.nathanielturner.com/juliuskambaragenyerere.htm Mohamed Said: Mwalimu in 1950s Dar (East African October 12 2008) Nyerere's remarks on Ali Hassan Mwinyi Corrupt practices PBS Interview with Nyerere on the Great Lakes crisis, December 26, 1996 Infed.org article on Nyerere and his views on education in Tanzania Jerry Atkin's Nyerere tribute, from InMotion Magazine SouthCentre Nyerere Memorial Site Mwalimu Neyerere Speeches A translation of Merchant of Venice into KiSwahili Nyerere Obituary from the ANC NPR Weekend Edition reflection on Nyerere Julius Nyerere Fellowship Nyererefoundation Called to greatness MercatorNet, 10 November 2006 Beatification inquiry for Tanzania's Nyerere (from Catholic World News) Is Nyerere's process to sainthood timely? (from IPP Media) The Julius Nyerere Intellectual Festival Week by Gacheke Gachihi, All Africa, 11 June 2009 The Julius Nyerere Master's Scholarships (University of Edinburgh) [fichua]omh Marais wa Tanzania [fichua]omh Pan-Africanism Administradors.png Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Julius Nyerere kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Jamii: Kurasa zinazotumia marudio ya hoja katika wito wa kigezoMbegu za wanasiasaWaliozaliwa 1922Waliofariki 1999Wanasiasa wa TanzaniaMarais wa AfrikaWatu wa historia ya TanzaniaMarais wa TanzaniaJulius Nyerere Urambazaji HujaingiaMajadiliano ya IP hiiMichangoUnda akauntiIngiaMakalaMajadilianoSomaTazama msimboFungua historiaTafuta Kutafuta Nenda Mwanzo Jumuia Matukio ya hivi karibuni Mabadiliko ya karibuni Ukurasa wa bahati Msaada Michango Miradi mingine Wikimedia Commons Chapa/peleka nje Tunga kitabu Pakua kama PDF Ukurasa wa kuchapika Vifaa Viungo viungavyo ukurasa huu Mabadiliko husika Pakia faili Kurasa maalum Kiungo cha daima Maelezo ya ukurasa Wikidata item Taja ukurasa huu Lugha zingine العربية English Español हिन्दी Bahasa Indonesia Bahasa Melayu Русский اردو 中文 55 more Hariri viungo Ukurasa huu umebadilishwa kwa mara ya mwisho tarehe 16 Mei 2019, saa 10:14. Maandishi yanapatikana chini ya leseni ya Creative Commons Attribution-ShareAlike License; matakwa mengine yanaweza kutakiwa. Tazama maelezo zaidi ya Matakwa ya Utumiaji.

Comments