Kutunga kwa ujauzito.
Uchavushaji hutokea pindi mbegu za kiume zinapofanikiwa kupenya kwenye yai la mwanamke. Wakati wa tendo la ndoa, manii ya mwanamume hutoka ikiwa na mamilioni ya mbegu, ila ni mbegu moja tuu itakayofanikiwa kupenya kwenye yai la mwanamke na kusababisha ujauzito. Baada ya kupenya, yai hujifunga na kukamilisha kitendo cha uchavushaji na hapo mimba huwa imeshatungwa (Conception). Pindi tuu mbegu ya mwanamume inapofanikiwa kuingia kwenye yai la mwanamke, jinsia ya mtoto huwa tayari imeshakamilika . Ikumbukwe kuwa, kwenye manii, kunakuwa na mbegu za kike na za kiume, na ni mbegu moja tuu ndiyo itakayofanikiwa kuingia kwenye yai, ama ya kike ama ya kiume. Hivyo, ni mbegu za mwanamume ndizo zinazoamua jinsia ya mtoto. Na
Siku tatu za mwanzo baada ya utungaji wa mimba, yai lililochavushwa hujigawa kwenye chembe hai nyingi. Hupita kwenye mirija ya fallopian(fallopian tube) na kupanda hadi kwenye mfuko wa uzazi (Uterus) na hujibadika hapo. Wakati huu, planseta au mji wa uzazi huanza kutengenezwa.
Maendeleo wiki ya 4
Wakati huu, mtoto anaanza kutengeneza umbo la muonekano wa sura pamoja na shingo. Moyo na misuli ya damu huanza kujengwa wiki hii. Kwa sasa, unaweza kutumia vipimo vya nyumbani kujipima na kupata matokeo halisi.
Maendeleo wiki ya 8
Hadi wiki hii, mtoto huwa na ukubwa wa nusu inchi (1.27cm). Pia, ngozi inayofunika macho (eyelid ) na masikio sasa yanaanza kutengenezwa, pia alama ya pua huanza kutokea kwa mbali. Mikono na miguuu tayari inakuwa imeshatengenezwa hadi sasa. Vidole navyo vinaanza kukua na kuonekana vyema.
Maendeleo wiki ya 12
Mtoto sasa anakaribia 5cm, na anaanza kuzunguka. Unaweza kuanza kuhisi juu ya mji wa uzazi (uterus). Kwa sasa, daktari anaweza kuanza kusikia mapigo ya moyo ya mtoto kwa kutumia kifaa maalumu. Hadi sasa, sehemu za siri za mtoto huwa zimeshajijenga vyema.
Maendeleo wiki ya 16
Ukubwa wa mtoto kwa wiki hii huwa kati ya 11cm hadi 12cm na uzito wa gram 100. Kwa wiki hii, mtoto anao uwezo wa kuchezesha macho, pia, moyo na mishipa ya damu inakuwe imeshakamilika. Vidole vyake sasa vinakuwa tayari vimeshatengeneza michirizi (fingerprints).
Meaendeleo wiki ya 20
Uzito wa mtoto sasa hufikia gram 285 na urefu wake huwa zaidi ya nusu rurla (15cm). Mtoto ana uwezo wa kunyonya vidole, kujinyoosha, muda si mrefu (kama bado haujaanza kusikia) utaanza kusikia akicheza "quickening."
Mara nyingi, ultrasound hufanyika wiki hii. Daktari atahakikisha kuwa mji wa uzazi (placenta) lipo salama na lina afya njema, pia atahakikisha kuwa mtoto wako anakua vyema. Kwa kutumia ultrasound, utaweza pia kuona mapigo ya moyo ya mtoto na baadhi ya viungo kama mikono, miguu na hata muenendo wa mwili wake.
Pia, wiki hii unaweza pia kutambua jinsia ya mtoto kama ni wa kike au wa kiume.
Maendeleo wiki ya 24
Sasa mtoto atakuwa na uzito zaidi ya nusu kilo, pia, anao uwezo wa kufuata sauti, unaweza kumsikia akizunguka kufuata sauti inapotokea. Jenga mazoea ya kuongea naye kuanzia sasa maana watoto hujenga mazoea na sauti wanazozisikia kila siku na huzitambua (kuonesha kuwazoea watu wenye sauti hizo) pindi wanapozaliwa. Wiki hii, sehemu za ndani za masikio (mfumo wa masikio) unakuwa umekamilika. Pia, anao uwezo wa kuhisi uelekeo wake ndani ya tumbo placenta.
Maendeleo wiki ya 28
Uzito wa mtoto kwa wiki hii unakaribia kilo moja, na huendelea kukua kwa haraka kwa wiki zijazo, mtoto hubadilisha sana uelekeo akiwa kwenye wiki hii. Kwa wale waliojifungua mtoto kabla ya muda, watoto waliozaliwa kwenye wiki hii, wana nafasi kubwa ya kuishi. Tafadhali ongea na daktari wako juu ya dalili za kujifungua kabla ya muda (preterm labor warning signs). Sasa, unatakiwa kuanza maandalizi ya kujifungua, maandalizi haya ni juu ya nini unatakiwa kufanya ukiwa leba, jinsi ya kumuhudumia mtoto mchanga nk. Pia, hakikisha unatembea na vifaa/taarifa muhimu popote unapoenda.
Maendeleo wiki ya 32
Wiki hizi, utamsikia sana mtoto akiwa anazunguka, na uzito wake hufikia hadi 1.8kg. Ngozi ya mtoto kwa wiki hii huonekana kama imejikunja kunja, kwa sababu, tabaka la fati huanza kutengenezwa. Kuanzia sasa mpaka unapojifungua, mtoto huongezeka uzito mpaka nusu ya uzito atakaozaliwa nao. Unaweza kuanza kuona majimaji ya njano yakitoka kwenye chuchu. Hii inaitwa colostrum, ni matayarisho ya kuanza kutenegeneza maziwa. Kuanzia wiki hii, ratiba ya kliniki hubadilika na sasa huwa kila baada ya wiki mbili.
Maendeleo wiki ya 36
uzito wa mtoto sasa hutofautiana, kuna sababu nyingi sana zinazopelekea utofauti huo kama jinsia ya mtoto (watoto wa kike huzaliwa na uzito mdogo kuliko wa kiume), idadi ya watoto (kama una mapacha, uzito hupungua) na pia maumbile ya wazazi. Hivyo, kitu cha msingi kuzingatia hapa ni uwiano wa ukuaji na siyo uzito halisi. Mtoto anaweza kuwa na uzito mdogo lakini amekuwa akiongezeka katika uwiano mzuri. Kwa wastani, watoto wengi huwa na urefu wa 47cm na uzito wa kilo mbili na zaidi katika wiki hizi. Ubongo sasa unajengeka kwa haraka zaidi. Mapafu nayo yanaelekea kukamilika na sasa mtoto anakuwa amegeuka na kichwa huwa kinaelekewa chini kwenye njia (pelvis).
Wiki ya 37 huchukuliwa kama ndiyo muhula wa kujifungua (term). Endapo utajifungua wiki ya 37-39 huchukulia kuwa umejifungua mapema, 39-40 huchukuliwa kama umejifungua katika muhula na wiki ya 41-42 huchukuliwa kama umechelewa. Watoto wengi waliozaliwa kabla ya wiki 39 huwa na nafasi kubwa ya kuwa na matatizo ya upumuaji na mengineyo, na kuna wakati wanahitaji uangalizi maalumu.
Kujifungua
Safari ya ujauzito huitimishwa wiki ya 40. tarehe ya kujifungua hukokotolewa kutokea siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho. Kulingana na mahesabu hayo, mwanamke kwa wastani hukaa na ujauzito kwa wiki 38 hadi 42, na muhula wenyewe hukamilika wiki ya 40 kwa sababu, inakadiriwa kuwa utapata ujauzito siku ya 14 baada ya hedhi yako ya mwisho. Mahebau haya huwa ni makadirio, hivyo kuna baadhi ya watoto huzaliwa wiki ya 42 na huchukuliwa kama ndani ya muhula.
Je upo katika harakati za kutafuta ujauzi basi wasiliana na doctar hapo juu
Comments
Post a Comment