Featured Post

Rasmi sasa Etienne kocha mkuu wa taifa stars sifa zote anazo soma zaidi....

                                                                                                                      
Ninachompendea huyu Etienne huwa anawachezesha wachezaji wetu kutokana na nafasi zao mechi na Rwanda alimuweka Makame dimba la chini namba sita mechi iliyofuata dhidi ya Sudan akampuzisha na kumuweka Mkude namba sita.Wakati Shomari Kapombe ilivyojulikana hatojiunga na timu jamaa akaamua kumuita Salum Kimenya azibe nafasi yake ukimuangalia Salum Kimenya ndiye beki namba mbili aliyekuwa na kiwango kizuri kwenye ligi kuu kwa sasa hivi nafikiri ana magoli kama matatu.Kama Paul Godfrey Boxer angekuwa fiti na siyo majeruhi na imani angemuita kama alivyofanya kwenye mechi ya kwanza ya kufuzu Chan dhidi ya Kenya alimuamini Paul Godfrey na alicheza mechi zote na alipeform ndiye beki namba mbili kwa sasa ukiacha Hassan Kessy wenye uwezo wa kuwa wabadala wa Kapombe.Acha kuhusu kuumia kwa Yondani nafikiri wengi tulikuwa tunajiuliza angecheza nani hila jamaa akaamua kumuamini Bakari Nondo beki kisiki wa Coastal Union.Huu ndio uzuri wake huyu jamaa anawatumia wachezaji kutokana na nafasi zao wanazocheza hautakuta hata mara moja akimuweka Feitoto namba sita wakati dogo nafasi yake ni namba nane dimba la juu.Kocha mzuri lazima ajue ubora wa wachezaji wake kwenye nafasi zao wanazocheza ndio maana aliamua kutuletea ingizo jipya Ditram Nchimbi akae pale mbele.Kuna vitu vingi alishaviona kushuka kwa kiwango kwa Salum Aiyeyeee pamoja na Ayooub Lyanga kuwa na kiwango cha kupanda na kushuka pamoja na kutokuwepo John Bocco.Kwa hili tumpongeze tu mzee maana anaonekana anawajua vizuri wachezaji wetu wa Kitanzania shida yetu sisi watanzania tunataka wachezaji wetu wacheze kama Brazil ,Uholanzi na Hispania hiko ni kitu ambacho hatuwezi tushukuru Mungu tumepata kocha anayejua kuwatumia wachezaji wetu vizuri kutokana na nafasi zao.Kuna makocha wengine walishindwa kabisa kujua hata nafasi za wachezaji wetu uwanjani hila huyu ameweza kwa Hilo nampa pongezi hata tukifungwa kama kikosi kakipanga vizuri unarizika maana tunajua uwezo wetu ndio umefikia hapo hongera Etienne kila la heri kwa kazi yako  mpya ya kuongoza Taifa letu la Tanzania  ðŸ’ªðŸ’ªðŸ’ªðŸ’ªðŸ’ªðŸ’ª

Comments