Featured Post

NILIVUNJA PENZI LANGU BILA KUJUA

๐Ÿ’”NILIVUNJA PENZI LANGU BILA KUJUA.(mapenzi donda lisilopona)๐Ÿ’”

๐Ÿš€๐Ÿ’ฅ๐Ÿ”ฅSEASON O2.๐ŸŒท๐ŸŒน๐Ÿ”

๐Ÿ‘‰SEHEMU 28.๐Ÿ‘ˆ       #Like_comment_share๐Ÿ’œ๐Ÿ’“๐Ÿ’Ÿ๐Ÿ’

ILIPOISHIA....
Bryson pamoja na mpenzi wake ambaye ni felista walikaa wote pale saloon kwa muda mrefu na hatimaye ilifika jioni wakaagana na kukubaliana kukutana kesho asubuhi wakati felista anaondoka kwenda shule ili waagane kwa mara ya mwisho na walipanga kuwa bryson awahi kuja saloon na felista mida ya saa tatu hivi na dakika zake asubuhi atapita pale saloon na kumuaga. Felista alikua na rafiki zake waliokua wakisoma wote shule moja waliotarajia kuondoka siku hiyo ambao ni christina, Jane pamoja na hasimu wake vero na ikumbukwe jane na vero walikua ni ndugu japo sio wa kuzaliwa na mama mmoja ila walikua ni wa baba mkubwa na baba mdogo hivyo basi kuna muda waliishi pamoja kwa bibi yao mzaa baba. Taratibu vero alianza kumpandikiza sumu jane ili amuone felista hafai kwa kumchukulia bryson wake kwahiyo kwa mbali urafiki wa felista na jane ukaingia doa kutokana na chuki za vero kwa felista.

  SASA ENDELEA NAYO..
Usiku mida kama ya saa mbili usiku bryson alikua tayari kafunga saloon yake na siku hiyo aliwahi kufunga saloon yake kwa sababu alitaka akapate muda wa kutosha wa kupumzika ili awasiliane na felista mpenzi wake vizuri na alipanga kuchati nae kuhusiana na mambo mengi ya kuyafanya wakati akiwa shule ili afanikiwe katika masomo vilevile kulitunza na kulilinda penzi lao, kwa upande fulani bryson alikua na huzuni na wivu ulimsumbua alipokumbuka atabaki mpweke pale saloon siku chache badae kabla ya kurudi chuoni kwake kwa sababu alizoea kukaa na kipenzi chake pale saloon mara kwa mara hivyo tayari alikua kashamzoea felista. Bryson akiwa njiani anarudi nyumbani huku akimuwaza felista alichukua simu yake na kumtumia felista ujumbe mfupi wa maneno kwa maana alijihisi kumkumbuka sana kisha akaendelea na safari yake.

Muda sio mrefu simu yake ilitoa sauti fulani hivi kuashiria kwamba kuna meseji ilikua imeingia kwenye simu yake na kwa kufanya haraka bryson alipekua simu yake katika sehemu ya meseji mpya zilizoingia katika simu yake huku akifikiria kichwani kwake kwamba itakua ni felista ndio kajibu meseji yake lakini alipofungua meseji mpya aligundua kuwa hakuwa felista aliyemtumia meseji ila alikua ni vero ndiye aliyekua kamtumia ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake. Kwa kiasi fulani bryson alighafirika kutokana na hali aliyokuepo nayo na kile alichokua akikifikiria kwa muda ule.. hivyo basi bryson aliamua kuipuzia ile meseji ya vero na badala yake akamtumia felista meseji nyingine ya pili baada ya kuona yupo kimya lakini muda ulipita bila felista kumjibu hatimaye bryson akafika nyumbani na moja kwa moja akaenda chumbani kwake kisha akaketi na kuanza kubadili nguo ili akaoge... Akiwa anaendelea na zoezi hilo mara simu yake ilianza kuita.

Bryson kuitazama alikuta ni vero ndiyo alikua kapiga, aliamua kuikata kwa sababu alikua na hasira vilevile alikua akimuwaza felista kwa sana. Vero aliendelea kupiga hadi bryson sasa akaona imezidi na hadi muda huu bryson alikua kasahau kwamba yeye mwenyewe alimwambia na kumuahidi vero kuwa usiku atamtafuta waongee zaidi ili amfahamishe zaidi kuhusu kilichomtokea lakini hakufanya hivyo na hakujali kwa sababu hisia za mapenzi zaidi kwa kipenzi chake felista zilimtawala na kwa siku hii ilikua ni siku ambayo bryson alijihisi upweke na kumkumbuka sana felista kwa sababu kichwani kwake alikua akiwaza kuwa kesho asubuhi felista ataondoka na mbaya zaidi hata meseji zake alikua hajajibiwa kitu kilichozidi kumchanganya kwani alihisi endapo wangechati hata kidogo basi mawazo na upweke ungepungua kwa kiasi fulani..

Baada ya vero kumpigia bryson mara kadhaa hatimaye simu ilipokelewa na kama kawaida bryson akiwa na hasira basi hupokea simu na kuendelea kuwa kimya kwa sababu huwa anafanya hivyo ili kujizuia kuongea vitu visivyostahili au visivyokua na maana nzuri na wala hilo halikumpa shida vero kwa sababu tayari upendo wake kwa bryson ulimsukuma sana kumnyenyekea bryson kwa kuwa aligundua kuwa anampenda sana na anamhitaji sana istoshe tayari alikua kashamkosea sana hivyo alihitaji kumuomba msamaha ili warudiane na huo ndio ulikua wakati ambapo alitakiwa kutumia vigezo vyote pamoja na njia zote ilimradi tu bryson amuelewe na kiukweli katika kipindi hiki vero alikua akiugulia maumivu makali ya mapenzi kwa sababu ni kweli alikua anampenda sana bryson na mbaya zaidi tayari bryson alikua ana mwanamke mwingine ambaye alikua ni rafiki yake na wanasoma katika shule moja kitu ambacho kilikua kikimuumiza sana vero na kumfanya ateseke sana ni basi hakuwa na jinsi ila kiukweli vero alikua hali wala kulala vizuri kwa sababu ya mawazo ya bryson na aliomba na kujipa imani ya kumpata bryson.

Vero alianza kwa kulalamika kiunyonge kwa kumuuliza bryson kwanini anamfanyie vitu vya ajabu na vya kikatili kiasi kile  istoshe tayari bryson mwenyewe alikua kamuahidi kuongea nae usiku pia vero alimuuliza bryson kwanini alikua akimkatia simu zake wakati alipompigia na istoshe meseji zake hakuzijibu kabisa... Bryson kwa unyenyekevu wake ambao siku zote ilikua ni kawaida yake hasa anapogundua kumkosea mtu basi hujishusha na alijikuta akimuomba msamaha vero na kumwambia vero kuwa sasa asijali yeye yupo tayari anamsikiliza kwahiyo vero aseme tote aliyopanga kumwambia kama walivyokubaliana walipokutana mchana kule nje ya saloon..

๐Ÿ’๐Ÿ’˜SOMA VIZURI MANENO HAPO CHINI๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡ YATAKUSAIDIA KUPATA MWENDELEZO๐Ÿ’œ๐Ÿ’ž๐Ÿ’–

ITAENDELEA......

JE NI NINI KILIFUATIA KWA BRYSON, VERO NA FELISTA???

USIKOSE SEHEMU 29 KATIKA SIMULIZI HII TAMU NA YENYE MAFUNZO KATIKA MAISHA.

๐Ÿ’ก✅Like na follow page yangu kwa kubonyeza link hii hapo chini๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

๐Ÿ‘‰https://www.facebook.com/pg/mariumwamigomba/posts/ ๐Ÿ‘ˆ

Kisha bonyeza alama ya dole gumba "๐Ÿ‘" kwa kufanya hivyo utapata posts zote za ukurasa huu haraka na kwa wakati kila zinapotolewa.

Pia unaweza kunifollow instagram kupitia link ifuatayo๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://instagram.com/mariummigomba?igshid=sz7d1hu7ksma

Comments