Featured Post

Nilivunja penzi pangu bila kujua season2 epsod 29

๐Ÿ’”NILIVUNJA PENZI LANGU BILA KUJUA.๐Ÿ’”

๐Ÿš€๐Ÿ’ฅ๐Ÿ”ฅSEASON O2.๐ŸŒท๐ŸŒน๐Ÿ”

๐Ÿ‘‰SEHEMU 29.๐Ÿ‘ˆ       #Like_comment_share๐Ÿ’œ๐Ÿ’“๐Ÿ’Ÿ๐Ÿ’

ILIPOISHIA....
Vero alianza kwa kulalamika kiunyonge kwa kumuuliza bryson kwanini anamfanyie vitu vya ajabu na vya kikatili kiasi kile  istoshe tayari bryson mwenyewe alikua kamuahidi kuongea nae usiku pia vero alimuuliza bryson kwanini alikua akimkatia simu zake wakati alipompigia na istoshe meseji zake hakuzijibu kabisa... Bryson kwa unyenyekevu wake ambao siku zote ilikua ni kawaida yake hasa anapogundua kumkosea mtu basi hujishusha na alijikuta akimuomba msamaha vero na kumwambia vero kuwa sasa asijali yeye yupo tayari anamsikiliza kwahiyo vero aseme yote aliyopanga kumwambia kama walivyokubaliana walipokutana mchana kule nje ya saloon..

SASA ENDELEA NAYOO...
Vero aliposikia hivyo alifurahi na ilikua ni kama vile fisi kakabidhiwa bucha au mbuzi kafia kwa muuza supu, kwa furaha isiyo na kifani vero alojisemea moyoni naanzaje kushindwa leo ikiwa Bryson kalainika kwangu kiasi hiki hadi kanipa nafasi ya kunisikiliza ili nijitetee kwake kwa makosa niliyomfanyia... Vero aliona ni bora sana na ni kheri kabisa endapo angemwambia ukweli Bryson kwanini alimsaliti na ni nini kilikua chanzo  change yote hayo. Vero alianza kwa kumwambia Bryson tafadhali naomba unisikilize kwa makini baba angu ili uweze tambua ukweli wa yote niliyoyafanya na nakuomba univumilie wakati nakuambia ukweli wote kwa sababu nimeridhia mwenyewe kwa kuwa ninakupenda sana na ninahitaji msamaha wako hivyo yanipasa kusema ukweli.

"Wakati huu tayari sasa Bryson alikua kwa kiasi fulani kajisahau kuhusu kuwa pengine felista anaweza kumtafta kwenye simu yake kwa kumpigia na kukuta simu yake ipo bize sana kwa muda mrefu kwa kuwa bryson alikua kajiandaa kusikiliza mkasa wote wa vero kitu ambacho kingechukua muda mrefu kukamilika", Bryson alimkubalia vero kwa shingo upande kwa sababu alichotaka kukusikia ni maneno ya vero kuhusiana na huo mkasa wake hivyo hakuhitaji kuweka vikwazo vingi kwa sababu angepoteza muda. Vero aliendelea kwa kusema, kama unakumbuka vizuri bryson Mwanzoni mwa penzi letu tulipendana sana na tulifurahi pamoja wakati ule kwa sababu wakati ule ulikua upo karibu sana na mimi na tulipata muda mwingi wa kulienzi penzi letu kwa sababu muda mwingi tulikua pamoja kwa kuwa ulikua hauendi saloon kwako kila siku na istoshe ulikua ukinijali sana kwa mawasiliano ili kunijulia hali endapo ntakua nipo mbali na wew hata kwa muda mfupi tu lakini nakumbuka baada ya hapo wote tuliporudi masomoni kwa kiasi fulani tulipotezana kwenye mawasiliano ila me sikujali nilijua lazima kungetokea ugumu kama huo kwa sababu ya masomo.

Likizo ilipoanza wewe uliwahi kurudi na me nilichelewa kwa sababu wazazi wangu waliniambia ni lazima nikawatembelee ndugu zangu ambao ni familia ya baba mdogo wangu sikuwa na jinsi ilinilazimu nifanye hivyo japo sikupenda kwa sababu tayari nilikua nakukumbuka sana pamoja na kulikumbuka sana penzi lako kitu ambacho kilinifanya niissshi kule kwa baba mdogo wangu kama vile nipo ukimbizini kwa kuwa sikuwa na furaha na amani ya moyo sababu ya penzi langu kwako. Siku zilienda nikajitahidi kudanganya sana ilimradi tu nipate nafasi ya kurudi nyumbani ili niweze japo kukuona bryson wangu na nakumbuka kwa kufanya hivyo baba mdogo wangu hakupendezwa kabisa na tabia yangu ila me sikujari kabisa sababu ya penzi langu la dhati na hisia nilizokua nazo kwako niliamua kuondoka kwa lazima bryson. Baada ya hapo nilifika nyumbani kwetu japo Nikita nimechelewa kidogo kwa sababu likizo ilikua imefika katikati na nilianza kukutafuta kama kifaranga aliyempoteza mama yake tena wakati wa masika ya mvua nyingi.

Nakumbuka ilikua ngumu kukupata kwa sababu tayari ulikua umebadili namba ya simu yako istoshe ulikua umebadili hata mtindo wa maisha nikimaanisha ratiba yako yaani ulikua ukiondoka asubuhi sana na mapema kwenda saloon kwako na kurudi usiku sana kama saa nne hadi saa tano usiku hivi, vilevile hata nilipokupata baada ya kusumbuka sana kukutafuta, basi kwa muda mchache tuliokua pamoja ilionekana kama tayari upendo wako ulikua umepungua sana  kwangu na ulijali sana ubize wako kuliko penzi letu kitu kilichopelekea kudolola sana kwa penzi letu hadi ikafikia kwa wiki tunaweza kukutana mara moja hivi kitu ambacho kilikua kinaniumiza sana moyo wangu na hata kama ni mawasiliano ya simu mpendwa wangu bryson ulikua hunipi muda wa kutosha wa kuongea na wewe yaani kidogo tu umekata et upo bize sana. Tuliendelea hivyohivyo na kama unavyojua mwenzako mimi ni mtoto wa kike nyumbani sitoki bila sababu maalumu muda mwingine nilikua nadanganya ili nipate muda wa kuja kwako lakini cha ajabu nikikutafuta unanijibu upo bize nikawa sina jinsi hivyo nikaona ni bora muda huo niweze kutoka na kwenda kwao rafiki yangu mirium.

Kiufupi ubize wako baba angu ulizidi japo nilijitahidi kuvumilia japo nilikua nikiumia sana lakini baadae nilianza kusikia maneno ya watu kuwa wewe hunihitaji tena na tayari ulishapata mwanamke mwingine ndio maana hunipendi na hunitaki tena ila unashindwa kuniambia tu, mbaya zaidi et huyo mtu uliekuwa naye kwenye mahusiano kama mpenzi wako tayari alikua ni rafiki yangu na mapenzi yenu mmeanza tangu wakati sijarudi... Jambo hili lilizidi kuniumiza na kunichanganya moyo wangu sana tena sana na nilipojitaidi kuchunguza rafiki yangu mirium alinambia hata yeye aliyasikia na ni ukweli ila akanishauri nisifatilie sana yataniumiza tu na hakuna kitakachonisaidia baada ya kujua na hapo ndipo mirium alipoanza kunishawishi nitoke kimahusiano na kaka yake anaeitwa white. Bila kuficha bryson kwa hali niliyokua nayo nilikua katika kipindi kigumu sana, mirium pamoja na white ndio watu pekee waliokua wakinifariji hivyo waliitumia fursa vizuri kwa sababu nilijikuta sina uwezo wa kupinga kuwa na white kwani mashambulizi yalizidi huku mimi nikiwa sina ulinzi wowote isipokua tayari nilikua nauguza majeraha uliyonipa moyoni.

๐Ÿ’๐Ÿ’˜SOMA VIZURI MANENO HAPO CHINI๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡ YATAKUSAIDIA KUPATA MWENDELEZO๐Ÿ’œ๐Ÿ’ž๐Ÿ’–

ITAENDELEA......

JE BRYSON ATACHOMOKA KWA VERO KWELI???

JE NI NINI KILIFUATIA KWA BRYSON, VERO NA FELISTA???

USIKOSE SEHEMU 30 KATIKA SIMULIZI HII TAMU NA YENYE MAFUNZO KATIKA MAISHA.

๐Ÿ’ก✅KUPATA HADITHI ZANGU ZOTE #LIKE "๐Ÿ‘" page yangu kwa kubonyeza link chini๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Kisha bonyeza alama ya dole gumba "๐Ÿ‘" kwa kufanya hivyo utapata posts zote za ukurasa huu haraka na kwa wakati kila zinapotolewa.

LMEDIA ON ISTAGHAM

Comments