Featured Post

SAFARI YA KUZIMU(2016/1979) episode 09 Mama Muuza

SAFARI YA KUZIMU(2016/1979)
episode 09
Mama Muuza pombe na mzee Ndonondo walibaki peke yao na kuanza kupanga mikakati ya kummaliza kijana Sudayi aliyewatia aibu mbele za watu!
"Sikochigaza mwana mdung'hu ayu we zuzi chilo che zuwali zomanyika du"(Hawezi kutusumbua mtoto mwekundu wa juzi huyu,usiku wa leo itafahamika tu")
Alisema Mzee Ndonondo akimwambia mama Muuza pombe kisha wakaagana na Mzee Ndonondo akalishika gogo lake kwa ncha ya kidole likatoweka kimaajabu!
****
Saa saba za usiku kwenye bwawa moja kubwa ambalo wanakijiji wa vijiji vya Vikonje,Buigiri na Chamwino hulitumia kunyweshea mifugo yao.Wenyeji.walikuwa wakiliita " Lamba lye mabwe" wakimaanisha bwawa la mawe maana lilikuwa na mawe ndani.
Usiku huo shughuli iliyokuwa ikifanyika ilikuwa ni ya kutisha zaidi!
Kijana mmoja aliyekuwa akitoka kijiji jirani cha Vikonje huku akiendesha baiskeli yake akielekea kijiji cha Chamwino alikokuwa akienda kununua miwa ili awahi kurudi kesho yake ambako kulikuwa na mnada!Mbalamwezi ilimdanganya aliamka na kuhisi huenda kunakaribia kukucha na ukizingatia miaka hiyo watu walikuwa wakiamini zaidi wanapoangalia nyota tu walijua kumekucha!
Kijana huyo wakati analikaribia bwawa hilo kwa mbali aliona moto mkubwa ukiwaka juu ya mawe yaliyokuwa katikati ya bwawa hilo kubwa!
"Mwene meso gangu au ng'hulota?" (Hivi ni macho yangu au naota?")
Alijisemea kijana huyo huku akiendeles kupigs pedali akilisogelea bwawa hilo kubwa. Kadiri alivyozidi kusogea ndivyo alivyozidi kuona mambo ya ajabu sana!akili yake ilikuja kurudi vyema na kuona mbalamwezi ilimdanganya huo haukuwa muda sahihi kwake kusafiri alipofika karibu kabisa na bwawa hilo na kuona watu wakiwa juu ya mawe hayo huku wakiuzunga moto mkubwa huku wakiwa uchi wa mnyama kabisa!
"Yuwiii napya nomuyenyu wachindi" (Uwiii nimeingia pabaya wanga hawa?")
Nguvu za kuendelea kuendesha baiskeli zilikwisha kabisa miguu iliingia ubaridi hakuweza kuendelea kupiga pedali akajikuta akisimamisha baiskeli yake,pembeni kulikuwa na mti mkubwa uliokuwa umezungukwa na majani na kutengeneza kichaka cha kutisha akaingia humo huku akitetemeka na kujihifadhi akiamini hajaonekana!Alikaa kiasi cha dakika tatu tu akaona mwanga wa kijinga cha moto ukimulikamulika huku ukija pale alipo na kisha ukafika moja kwa moja na kuingia pale alipojificha kisha mkono mkubwa wa baridi sana ukamshika!
"To uze kuno" (hebu njoo huku)
Kijana huyo alihisi kama ganzi ya ajabu ikimuingia mwilini,hakuna alichoweza kukifanya tena alitaka kuongea lakini hakuweza
ITAENDEL

Comments