Featured Post

Kampuni ya Volkswagen ina mpango wa kufunga Viwanda vyake vitatu

Kampuni ya Volkswagen ina mpango wa kufunga Viwanda vyake vitatu nchini Ujerumani na kupunguza maelfu ya Wafanyakazi. Aidha, ukubwa wa Viwanda vitakavyobakia nao upunguzwa. Kampuni hiyo ya utengenezaji Magari ambayo ndio kubwa barani Ulaya imetumia wiki kadhaa sasa ikifanya majadiliano na vyama vya Wafanyakazi kuhusu mipango yake ya kibiashara na kupunguza gharama. Volkswagen iko kwenye wakati mgumu kiuchumi, kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kuongezeka kwa gharama za nishati, ushindani mkubwa kutokea barani Asia na kudhoofika kwa mahitaji ya bidhaa zao barani Ulaya na China. Volkswagen, ambayo ina takribani wafanyakazi 300,000 nchini Ujerumani na inayosimamia viwanda 10 imesema itatoa mapendekezo yake ya namna ya kupunguza gharama za wafanyakazi ifikapo Jumatano wiki hii katika mkutano ambapo wafanyakazi na utawala watakutana kwa mara pili ili kuendelea na majadiliano. #KitengeUpdates

Comments