Featured Post

mkuu wa majeshi afariki

Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Musuguri, amefariki Dunia leo, Oktoba 29, 2024, jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu. Jenerali Musuguri, aliyezaliwa Januari 4, 1920 huko Butiama Mkoani Mara, aliitumikia Nchi katika Jeshi kuanzia Mwaka 1942 hadi 1988, akihitimisha Uongozi wake kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kati ya 1980 na 1988. Alianza kazi yake kijeshi katika King’s African Rifles (KR) na Tanganyika Rifles kabla ya kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Jenerali Musuguri aliongoza majeshi ya Tanzania katika vita dhidi ya Idi Amin Dada wa Uganda Mwaka 1978, baada ya uvamizi wa eneo la Kyaka, Mkoani Kagera. Mapambano na vita alivyoshiriki ni pamoja na Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Battle of Madagascar, Vita vya Kagera, na Battle of Simba Hills Kusoma Historia zaidi ya Jenerali Musuguri, bofya hapa https://jamii.app/RipGeneralMusuguri #JamiiForums #RIPGeneralMusuguri #JFMatukio

Comments