Featured Post

SABABU ZA VINICIUS JR KUKOSA TUZO HIZI HAPA.......! Rodri ameibeba Ballon d’Or

SABABU ZA VINICIUS JR KUKOSA TUZO HIZI HAPA.......! Rodri ameibeba Ballon d’Or kama masihara vile watu wengi hawaamini kama mwamba amebeba, lakini hapa naomba niseme jambo kabla haujakutana na washikaji zako na kuleta ubishi usio na maana. Hizi ni kura ambazo zimepigwa na makocha, makepteni wa timu za taifa na waandishi wa habari. Sasa sio ukae hapo halafu uwadanganye watu kwa kusema kwamba mtu amependelewa. Hizo ni tuzo ambazo zinapigwa kura na watu, hata wewe ungewekwa, ungeweza kunipigia Nyemo kama tu nipo hapo. Sasa baada ya hapo, wanaangalia nani kapata nyingi na nani kapata kidogo. Hizi tuzo ni za mapenzi, unaweza kufanya kazi kubwa, usifunge mabao mengi lakini bado ukaibeba bila matatizo, inategemea na watu wanakupenda vipi. Why Vini amekosa? Nadhani ni kwa namna mwenyewe alivyojiweka kwamba mtu fulani anayependa sana kulalamika, anayependa kuwaambia wenzake maneno mabaya. Vini ukimbagua, analalamika ila yeye kukutolea maneno ya kashfa, kwake imekuwa kawaida. Just imagine alimwambia mpaka De Paul kwamba yeye ni bingwa wa klabu bingwa, akasahau kwamba mwamba ni bingwa wa dunia. Juzi wakati walipofungwa na Barcelona, alimfuata Pedri na kumwambia “Nitashinda Ballon d’Or” So yeye hapendi kutolewa maneno machafu ila yeye anapenda kuwatolea watu maneno machafu. Wengine wataingiza masuala ya ubaguzi bila kukumbuka kwamba George Weah aliishinda hii tuzo. Watasahau kwamba Zidane, pamoja na kuwa na asili ya uarabuni, bado akashinda. Ronaldinho na wengine wengi. As barcelona fan, nimefurahi, tena sana, yaani sana. Nimefurahi kuona Vini akiumia, tena si yeye tu, hata kama angekuwemo Mbappe, Rodyigo na wengine, bado ningefurahi. Nadhani waliopiga kura nao wameangalia, yaani wampe kura mtu mwenye nidhamu mbovu kama huyu? Wamemkataa mazima. Ila Rodri...ile mashine achana nayo kabisa, ile ni pumzi ya City na Spain, yaani akikosekana tu, unajua kuna mtu hayupo. Huyu jamaa ameshinda nini? Ameshinda haya hapa chini. Kombe la Ligi ya England. Kombe la Carabao. Kombe la Ulaya. Vini (Bingwa wa kulialia) ameshinda.... Kombe la Ligi ya Hispania Kombe la Super Cup Kombe la Klabu Bingwa Big up Rodri. Poleni mashabiki wa Real Madrid....hizi siku 10 ni za maumivu makali sanaaaa.

Comments