Featured Post

why GONGA94 Take over Tanzania

Aliyekuwa meneja wa vipindi Times FM katika mahojiano na Mwanaspoti

Dawnload videos
find girls from your country Aliyekuwa meneja wa vipindi Times FM katika mahojiano na Mwanaspoti amesema tofauti na wengi walivyokuwa wakidhani, Didah Shaibu kwa mara ya kwanza alienda Times FM mwaka 2003 kama mwanafunzi wa mafunzo kwa vitendo(field) akitokea chuo cha uandishi wa habari ambapo Dida alikuwa na umarekani flani ikiwemo kupenda muziki wa RnB na hip hop kutoka Marekani hivyo kutaka kutangaza kipindi cha aina hiyo na sio taarabu au mambo ya uswahilini Amesema Diddah hakuwa shabiki wa mambo ya taarab kabisa lakini kutokana na ucheshi, uchangamfu na uchapaji kazi wake wakaamua wamuajiri moja kwa moja na kumuelekeza zaidi kazi Meneja amesema kwa wakati huo radio nyingi za Tanzania kuanzia mchana hadi jioni radio zilitawaliwa na vipindi vingi vya muziki wa nje hivyo yeye na kiongozi mwingine wa Times FM wakapendekeza waanzishe kipindi cha muziki wa taarab na katika kufanya tathmini nani atangaze waliona Didah atafaa kwakuwa ni mtu mwenye asili ya pwani mkoa wa Tanga. Didah alisita na kuwaambia hataweza kwasababu yeye sio mfuatiliaji wa taarabu lakini wakampa moyo kuwa ataweza Dida alianza kipindi cha "Mitikisiko Ya Pwani" ambapo ndani ya muda mfupi kikawa maarufu wakakiongezea muda ukawa hautoshi, wakakiongezea tena muda hadi saa nne kwa siku kuanzia mchana hadi jioni na baadaye kuwa kipindi mchana hadi jioni kilichotokea kupendwa zaidi na kufuatiliwa na wengi kuliko radio zote kwa mujibu wa utafiti huru uliofanywa wakati huko na baadaye Dida kupewa tuzo, na wadhamini kujitokeza wa kutosha kwenye kipindi hicho Meneja amesema Dida alisaidia sana kuukuza muziki wa taarabu na hata kuongeza ubora katika muziki huo kwasababu alikuwa anakataa kupiga nyimbo za taarabu zisizokuwa na ubora na hata baadhi ya wasanii wa muziki huo walipolalamika kuwa anawabania Dida aliweka wazi kuwa baadhi yao kazi zao hazikuwa na ubora hivyo vikao vikaitishwa na wasanii wa taarabu na Times FM kuhusu kuongeza ubora wa kazi zao Meneja amesema Dida alikuwa anathamini wengine akiona mtu ana uwezo wa kitu fulani ili apewe nafasi. Kwa mfano amesema Dida ndie alianza kupendekeza Dr.Kumbuka awe msaidizi wake baada ya kumuona mtaani akiwa na uwezo huo Kabla ya kugeukia utangazaji na kuwa maarufu, Didah aliwahi kuwa muigizaji wa tamthilia katika kundi la uigizaji la Kaole Sanaa Group lililotamba wakati huo na kuibu mastaa wengi japo yeye uigizaji haukumtoa Didah alifariki wiki kadhaa zilizopita na kuacha pengo katika tasnia ya utangazaji

Comments