Featured Post

Wasifu wa Grace Mapunda umeminywa sana isivyostahili anavyoelezewa ni kana kwamba alianza sanaa juzi juzi baada ya kuigiza tamthilia ya Huba na wengine wanamuandika kuwa ni maarufu kwa jina la Tessa yaani kupitia Huba inayooneshwa kwenye kisembuzi kimoja pekee hivyo tuseme hakuwa akijulikana kwa ukubwa kabla !!

Ukiangalia kwa asilimia 95% kwenye mitandao na mainstream media zetu Wasifu wa Grace Mapunda kisanaa na kikazi kwa ujumla hajatendewa haki sijui ni tatizo la waandishi kuwa wavivu, kutofanya utafiti kuhusu mhusika au lah ! Wasifu wa Grace Mapunda umeminywa sana isivyostahili anavyoelezewa ni kana kwamba alianza sanaa juzi juzi baada ya kuigiza tamthilia ya Huba na wengine wanamuandika kuwa ni maarufu kwa jina la Tessa yaani kupitia Huba inayooneshwa kwenye kisembuzi kimoja pekee hivyo tuseme hakuwa akijulikana kwa ukubwa kabla !! Lakini kiuhalisia Grace Mapunda tayari lilikuwa jina kubwa kisanaa kabla ya tamthilia husika yenye takribani miaka 7 tangu ianze kuoneshwa Grace yupo machoni pa wengi kisanaa si chini ya miaka 20 sasa na wengi tulianzia kumjulia kupitia kundi la Shirikisho Msanii Afrika kupitia tamthilia zao ITV kipindi ambacho ITV ilikuwa inaonekana bure kwa kila mwenye TV haikuhitaji kisembuzi chochote hivyo kuonwa na wengi Baada ya hapo filamu zikapamba moto na yeye kuigiza filamu zisizopungua hata 70 muda mwingi akiwa busy location. Filamu nyingi alizoigiza zilikuwa maarufu na wasanii wengine maarufu wakiwemo kina Kanumba, Ray, Wema, Uwoya, Wolper na wengineo maarufu Sasa msanii kama huyu baada ya kifo chake, anavyotambulishwa utafikiri alianza kuigiza miaka 7 iliyopita Nafikiri katika kamati maalum ya mazishi au hata contents kwa media ilipaswa kuwepo video fupi rasmi na maalum inayomuonesha Grace alikoanzia kisanaa miaka hiyo hadi alipofikia sasa kisanaa kama sehemu ya kumuenzi kwa kutuburudisha, kutuonya, kutuadhibu na kutuelimisha kupitia kazi zake za sanaa maana media nyingi kubwa zimeshindwa hata kujiongeza katika hilo hivyo kizazi cha watoto na vijana wa sasa kuwa rahisi kudhani kaanza juzi sanaa Grace alikuwa mmoja wa waigizaji wazuri wenye vipaji ambaye hachoshi kirahisi kumtazama katika filamu au tamthilia Hii sio kwa Grace Mapunda pekee kuna wasanii walishatangulia mbele ya safari na wao walipaswa kupewa heshima kama hiyo kisanaa katika kuwaelezea kikazi walikoanzia ila haikuwa hivyo Tujifunze na turekebishe Pumzika kwa amani Grace Mapunda https://youtu.be/aMN10kc43BY?si=tEzH8fmOEPBldWRx

Comments